MIRADI YA MAJI TABOR...
MIRADI YA MAJI TABORA YAMNG'ARISHA Mhe. AWESO MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.
01 Aug, 2025
MIRADI YA MAJI TABORA YAMNG'ARISHA Mhe. AWESO MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

Katika kupitia miradi ya maendeleo Mkoani Tabora Mwenge wa Uhuru umetua Wilayani Igunga ambapo mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya Ziwa Victoria unaosimamiwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Igunga umezinduliwa.

Ndugu Ismail Ali Ussi kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2015 baada ya kukagua na kutembelea mradi huo amesema ameridhika na kisha kuuzindua.

Ikumbukwe mradi huu wa Makomero - Mgongoro uliwekewa jiwe la msingi na Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa (MB) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 12.03.2025

"Wenzetu wa Mamlaka za maji na RUWASA wanafanya vizuri sana kupitia wizara ya maji kwa kutoa huduma bora kwa wananchi, kila halmashauri Tabora tumepitia miradi ya maji na imefanya vizuri" Ismail Ali Ussi ameyasema hayo Igunga alipokuwa ana zindua mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi ya Ziwa victoria kutoka Makomero - Mgongoro.