MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA TABORA (TUWASA) IMEWAFIKISHA MAHAKAMANI WATEJA WENYE MADENI SUGU YA MAJI.
25 Sep, 2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) kupitia Kitengo cha Sheria imeendelea na zoezi la kuwafikisha mahakamani wateja wenye madeni sugu wanaohudumiwa katika Wilaya ya Tabora.
Leo tarehe 25/09/2025 kesi za wateja 09 zitaendelea kusikilizwa. Hadi sasa wateja wasiopungua ishirini na tano(25) wameshafikishwa mahakamani.
Aidha baadhi ya wateja wamekubali uhalali wa madeni na kuahidi kulipa wakati wengine wameingia mkataba na Mamlaka kulipa ndani ya muda uliowekwa kisheria.
Mwisho, kuna baadhi ya wateja wamepewa muda wa siku kadhaa na Mahakama kufanya malipo na kufika kortini wakiwa na risiti zao halali za malipo na kwa watakaoshindwa kulipa kama walivyoahidi kesi zao zitasikilizwa na mahakama kisha kutolewa uamuzi.