KAMATI YA BUNGE YA K...
KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA MAJI NA MAZINGIRA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BWAWA LA KIZENGI WILAYANI UYUI.
15 Mar, 2025
KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA MAJI NA MAZINGIRA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BWAWA LA KIZENGI WILAYANI UYUI.

Kamati ya Mazingira ya Bunge ikiongozwa na Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) Mwenyekiti wa Kamati hiyo imekagua ujenzi wa bwawa la maji la Kizengi wilayani Uyui, ambalo linatarajiwa kunufaisha wakazi 90,000 na utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 60.

Pamoja na mafanikio ya mradi huo, imeelezwa kuwa kuna changamoto ya upatikanaji wa fedha ili kumalizia mradi huo.

Baada ya kukagua mradi huo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) alieleza kuridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la Kizengi na kuwapongeza wataalam wa Wizara ya maji wakiongozwa na Mhe. Jumaa Aweso (Mb) kwa kuhakikisha huduma ya majisafi inafika kwa wananchi.

Kwa ujumla Kamati imetoa shukran kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi huu wa uchimbaji wa bwawa la Kizengi ili kufanikisha upatikanaji wa majisafi kwa wananchi.