KAMATI YA PAC YAPONG...
KAMATI YA PAC YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA AWAMU YA 1 & 2 TABORA.
18 Mar, 2024
KAMATI YA PAC YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWA AWAMU YA 1 & 2 TABORA.

Kamati ya PAC ikiongozwa na Mhe. Japhet N. Hasunga (Mb) ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati imepokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa awamu ya 1 & 2 kutoka kwa Eng. Edward Tindwa kutoka Wizara ya Maji na Taarifa ya hali ya huduma ya maji Manispaa ya Tabora, Sikonge, Urambo, Kaliua na Isikizya iliyotolewa na Eng.Mayunga Kashilimu - Mkurugenzi Mtendaji TUWASA.

Kamati ilitembelea mradi wa maji kwa kufika katika Tenki kubwa la maji la Itumba lenye ujazo wa lita milioni 9 lililopo kata ya Uyui Kijiji cha Timkeni Manispaa ya Tabora na Tenki la Kazehill lenye ujazo wa lita milioni 5 ambalo lipo kata ya Kitete ambapo matenki hayo yamejengwa kupitia mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.

Baada ya majadiliano kamati imetoa maelekezo yafuatayo;-

Kamati imepongeza utekelezaji wa mradi huu na imeelekeza upotevu wa maji upungue, usimamizi wa huduma uongezeke na madeni ya Taasisi za Serikali yafuatiliwe.

“Hii ni Kamati ya Usimamizi tunapima thamani ya pesa, yaani kama malengo ya mradi yamefikiwa ikimaanisha  huduma ya maji kuwafikia wananchi.” Mhe. Japhet N. Hasunga (Mb).

Mwisho kabisa Bw. Dick Mlimuka ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TUWASA ameiambia kamati kuwa maelekezo yote ameyapokea kwa ajili ya utekelezaji na ameishukuru kamati kwa ujio wake katika Mradi huu wa Maji kutoka Ziwa Victoria.