MHE. JUMAA H. AWESO ATOA MAELEKEZO KWA MKANDARASI MEGHA ENGINEERING & INFRASTRUCTURE LTD KUKAMILISHA KWA WAKATI MRADI WA MAJI MIJI 28 SIKONGE, URAMBO NA KALIUA – TABORA.

Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (MB) Waziri wa Maji ameambatana na Bi Mwajuma Waziri Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji katika ukaguzi wa mradi wa maji miji 28 Sikonge, Urambo na Kaliua.
Kabla ya Ziara kuanza walifika na kuzungumza na Mhe. Paul Chacha Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye alisema kuhusu huduma ya maji Tabora hana lawama na TUWASA.
Mhe. Aweso amekagua ulazaji wa bomba eneo la Kiwanda cha nyuzi ambao hauhusishi kukata barabara ya lami (horizontal directional drilling), tenki la maji la Kalemela B kwa ajili ya wakaazi wa Kaliua lililopo Urambo na tenki la maji la Sikonge.
Aidha Mhandisi Mayunga Kashilimu Mkurugenzi Mtendaji TUWASA amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa maradi huo Kalemela B Urambo ambao umefikia asilimia 71ambapo kwa sasa upatikanaji wa maji mjini katika Mkoa wa Tabora ni wastani wa 89.8% ambapo Isikizya na Manispaa ya Tabora ni 97%, Sikonge 40.5%, Urambo24.5% na Kaliua 35%.
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya za Sikonge, Urambo na Kaliua wameshukuru kwa mradi huu ambao utaleta faraja kwa wakaazi wa maeneo yao na kuahidi kuusimamia vema ili wananchi watuliwe ndoo kichwani kama alivyokusudia Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumtua mama ndoo kichwani.
Mhe. Aweso amesema miradi hii ya miji 28 ni kielelezo cha mahusiano mazuri kwa wananchi na amemuagiza mkandarasi Megha & Infrastructure LTD kuacha visingizio afanye kazi usiku na mchana wananchi wapate maji ifikapo Octoba 2025 kwakuwa fedha za miradi hii zipo zaidi ya trillion moja ili kutimiza dhamira ya Mhe.Rais ya kumtua mama ndoo kichwani na kuvuka lengo la upatikanaji wa maji mijini 95% na vijijini 85%.
Pia amewasisitiza wasimamizi wa miradi hii kuhakikisha kunakuwa na ushirikishwaji wa wananchi na viongozi wa maeneo inapotekelezwa miradi hii ya miji 28.