MHE. JUMAA H. AWESO AFANYA UTEUZI WA WAKURUGENZI WATENDAJI WATATU WAKATI WA UKAGUZI WA MRADI WA MAJI MIJI 28 SIKONGE, URAMBO NA KALIUA – TABORA.
17 Jul, 2025

Mhe. Jumaa Hamidu Aweso (MB) Waziri wa Maji alipokuwa anaendelea na kazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 Tabora amefanya uteuzi wa Wakurugenzi watatu wa Mamlaka za Maji ambapo;
Amemteua Bw. Alexander Ntonge (TUWASA) kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Igunga.
Mhandisi Humprey Muyombela (IGUWASA) kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Nzega na Mhandisi Laurence Wasala (KASHWASA) kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji Busega.
Amewataka kuchapa kazi kwa weledi na kuhakikisha lengo la kuwapa wananchi maji linatimia.