KATIBU MKUU WIZARA Y...
KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI ATETA NA WATUMISHI SEKTA YA MAJI - TABORA
11 Oct, 2024
KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI ATETA NA WATUMISHI SEKTA YA MAJI - TABORA

Eng Mwajuma Waziri Katibu Mkuu wa Wizara ya maji leo amezungumza na watumishi wa sekta ya maji Tabora baada ya kazi ya uwekaji wa jiwe la msinngi katika mradi wa maji wa miji 28 Sikonge - Tabora uliofanywa na Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Eng Mwajuma amewapongeza watumishi wa sekta hii na kuwaambia wajenge utaratibu wa kukutana, kufahamiana na kufanya kazi pamoja kama timu. Amesema kuwa pongezi ambazo Viongozi wa Wizara ya maji wamepata kutoka kwa Mhe. Dkt Philip Mpango  zimetokana na uchapa kazi wa watumishi wa sekta ya maji Tabora hivyo amewapongeza sana.

Pia amesisitiza kufanya kazi kama timu, kufanya kazi kwa weledi na kuendelea kujifunza kwani teknolojia inabadilika kila wakati, maafisa utumishi wasikikize malalamiko ya watumishi na kufanyia kazi, viongozi wafanye succession plan ili kuwaandaa watumishi wanaowasimamia kuwa viongozi .

Mwisho aliwaagiza watumishi wote kuhakikisha majisafi na salama yanapatikana kwa wananchi na ambao hawajafikiwa na mtandao wa maji wataalam wafanye mchakato kuhakikisha wanapata maji safi na salama bila kusahau kuendelea kuimarisha umoja katika utendaji.