MWENGE WA UHURU WAPO...
MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI TABORA, TUWASA YASHIRIKI MAPOKEZI.
26 Jul, 2025
MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI TABORA, TUWASA YASHIRIKI MAPOKEZI.

Mapema leo tarehe 26.07.2025 TUWASA imeshiriki makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Uyui- Tabora kutoka Singida ambapo Mhe. Paul Chacha Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliupokea kutoka kwa Mhe. Halima Dandego Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Tura iliyopo Uyui - Tabora.

Mwenge wa Uhuru utafikia Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 38.8 Mkoani Tabora.

Kauli mbiu" Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu".