BODI YA EWURA YAHITI...
BODI YA EWURA YAHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI TUWASA.
21 Feb, 2024
BODI YA EWURA YAHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI TUWASA.

Bodi ya EWURA imezielekeza Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira  nchini kutathmini huduma  kwa wateja wake ili kupata mrejesho utakaozisaidia kuboresha utendaji na huduma zao.

Bodi hiyo, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Mark Mwandosya, imetoa maelekezo hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake TUWASA.

“Kwa niaba ya Bodi, napenda kuwakumbusha TUWASA na mamlaka zote za maji nchini kutathmini huduma zinazotolewa kwa wateja, fanyeni utafiti wa namna wateja wanavyoridhishwa na huduma zenu ili muweze kupima utendaji wenu” Alisisitiza.

Mwenyekiti wa Bodi ya TUWASA, Bw. Dick Mlimuka ameihakikishia Bodi ya EWURA kuyatekeleza maelekezo yaliyotolewa ili kuendelea kuleta tija kwenye huduma za maji na usafi wa mazingira mjini Tabora.