Eng. MAYUNGA AKAGUA...
Eng. MAYUNGA AKAGUA BOMBA LA KUPELEKA MAJI SIKONGE, MRADI WA MAJI MIJI 28.
20 Oct, 2025
Eng. MAYUNGA AKAGUA BOMBA LA KUPELEKA MAJI SIKONGE, MRADI WA MAJI MIJI 28.

Mkurugenzi Mtendaji Eng.  Mayunga A. Kashilimu amekagua utekelezaji wa mradi wa maji kupeleka Sikonge, Urambo na Kaliua ambapo ametembelea sehemu ambayo bomba la maji limevushwa kwenye barabara kwa njia ya Horizontal directional drilling eneo la Miemba kwenda Sikonge.

Pia Eng. Mayunga amekagua eneo la Malolo ambapo bomba za maji zinaachana kupeleka maji Sikonge na lingine kupeleka Urambo hadi Kaliua kutoka Manispaa ya Tabora.

Mwisho Eng. Mayunga ametembelea tenki la maji la Sikonge ili kujiridhisha na upatikanaji wa maji ya Ziwa Victoria kupitia mradi huu.

Eng Mayunga amempa maelekezo ya kusisitiza Mhandisi Mshauri WAPCOS LTD kuhakikisha maji yanapatikana na Mhandisi Mshauri ameeleza kuwa mwezi huu Oktoba, 2025 Sikonge watapata maji na baadaye Urambo na Kaliua.

Ikumbukwe kuwa tayari bomba kubwa la maji kutoka Ziwa Victoria lililopo Manispaa ya Tabora limeungwa na bomba kubwa kwa ajili ya kupeleka maji Sikonge na Urambo kisha Kaliua. Na pia mradi huu unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 143.26 unatarajia kuhudumia wakaazi 490,926 mara utakapokamilika.