DKT. PHILIP ISDOR MP...
DKT. PHILIP ISDOR MPANGO MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA MAJI WA MIJI 28.
11 Oct, 2024
DKT. PHILIP ISDOR MPANGO MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA MAJI WA MIJI 28.

Dkt. Philip Isdor Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wa miji 28 ambao unapeleka maji ya Ziwa Victoria kwenda  Miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua. Jiwe la msingi limewekwa wilayani Sikonge.

Mradi huu unagharimu fedha kiasi cha shilingi bilioni 143 na ukikamilika Oktoba 2025 upatikanaji wa maji kwa miji hiyo utafikia asilimia 95.

Alikuwa pamoja na Eng Kundo Mathew ( mb) Naibu Waziri wa Maji,  Mhe. Paul Chacha Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Eng. Mwajuma  Waziri Katibu Mkuu - Wizara ya Maji.