SALAM ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2024 KWA WATEJA WA TUWASA

Eng Mayunga Kashilimu - Mkurugenzi Mtendaji, Benard Biswalo - Mkurugenzi huduma kwa wateja na Najibah Batenga katika kipindi cha Meza Huru kinachorushwa na Redio VOT wamezungumza mambo matatu kwa wateja wao kama ifuatavyo;-
Shukrani kwa wateja kwa ushirikiano waliotoa kwa kipindi chote cha mwaka 2023 kwa kutumia maji safi na salama ya TUWASA, kulipia bili za maji, kutoa taarifa mbalimbali kuhusu huduma ya maji, kutoa maoni ya kuboresha huduma ya maji Tabora na zaidi kuwa wavumilivu kipindi cha changamoto ya huduma.
Wamewasisitiza wateja wote waliokatiwa maji warejeshe kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu kwa kutumia fursa ya kuondolewa malipo ya faini na wananchi wasio na maji majumbani wajiunge na huduma ya maji.
Wametoa shukrani zao kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha za mradi wa maji wa miji 28 maji kutoka Ziwa Victoria kwenda miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua unaogharimu kiasi cha fedha bilioni 145.9 na utekelezaji unaendelea umefikia asilimia 26 na pia fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kutekeleza mradi wa majitaka Tabora Manispaa unaoendelea ambao umefikia asilimia30.
Kwa umuhimu mkubwa wamewatakia wateja wote wa TUWASA na watanzania kwa Ujumla Heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2024 wenye mafanikio.