BILIONI 143.2 KUFIKI...
BILIONI 143.2 KUFIKISHA MAJI YA ZIWA VICTORIA SIKONGE, URAMBO NA KALIUA.
31 Jul, 2023
BILIONI 143.2 KUFIKISHA MAJI YA ZIWA VICTORIA SIKONGE, URAMBO NA KALIUA.

Wakandarasi wa mradi wa Maji wa Miji 28 wamekabidhiwa mradi huo mbele ya wakaazi wa Urambo wakati wa tamasha la Samia Festival lililoandaliwa na Mhe. Kenani Kihongosi Mkuu wa Wilaya ya Urambo.

Mradi huo unatarajia kuleta maji kutoka Tabora Manispaa hadi miji ya Sikonge, Urambo na Kaliua na  kukamilika kabla ya mwaka 2025 ambapo changamoto ya maji iliyopo katika miji hiyo itakwisha kabisa.

Mhe. Jumaa  Hamidu Aweso (Mb) Waziri wa Maji amewaeleza wananchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta suluhu ya changamoto ya Maji katika Wilaya za Urambo, Kaliua na Sikonge kupitia mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.

Pia Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe Magret Sita na Mkuu wa Wilaya ya Urambo Kenani Kihongosi wamempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuleta maendeleo makubwa ndani ya Wilaya ya Urambo katika Maji, Afya, Elimu, Umeme, Miundombinu, Kilimo na Uchumi.