MAFANIKIO YA SERIKAL...
MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA HUDUMA YA MAJI TABORA NA PROMOSHENI ZA WIKI YA MAJI MACHI, 2024.
20 Mar, 2024
MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA HUDUMA YA MAJI TABORA NA PROMOSHENI ZA WIKI YA MAJI MACHI, 2024.

Leo tarehe 20.03.2024 Bw. Benard Biswalo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TUWASA na  Bi Najibah Batenga ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma katika kipindi cha Kifungua kinywa kupitia Redio Uyui wameelezea Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya sita katika huduma ya maji Tabora na  Promosheni za wiki ya maji kwa wateja waliokatiwa maji.

Ameeleza Bw. Biswalo kuwa wateja wote waliokatiwa maji na wana madeni yasiyozidi shilingi 100,000/=  watatakiwa kulipa deni lote bila faini na kurejeshewa huduma ya maji na Wateja wote waliokatiwa maji na wana madeni ya zaidi ya shilingi 100,000/=  watatakiwa kulipa nusu ya deni bila faini na kurejeshewa huduma wakati nusu nyingine watamalizia kulipa kwa awamu kipindi cha miezi mitatu.

Ameeleza kuwa promosheni hii inaisha muda wake tarehe 31.03.2024 wateja wachangamkie fursa hii kwa kuepuka kufikishwa mahakami kwa ajili ya kutolipa madeni yao.

Bi Najibah pia ameeleza mafanikio ya miaka mitatu ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Sekta ya maji hasa Tabora kwamba ametoa fedha za miradi ya maji Bilioni 149 ambazo zimesaidia asilimia 95 ya wakazi wa Manispaa ya Tabora kupata huduma ya majisafi na salama na ifikapo Octoba,2025 maji yatakuwa yamepatikana Kaliua, Sikonge na Urambo baada ya mradi kukamilika ambao unaendelea wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria maeneo hayo na kumaliza changamoto ya maji na hadi sasa utekelezaji wake umefikia  asilimia 34.

Kauli Mbiu wiki ya maji Machi,2024

“UHAKIKA WA MAJI KWA AMANI NA UTULIVU”