TAARIFA YA UPUNGUFU...
TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
08 Dec, 2023

TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI

Ndugu wateja wetu.

Nawajulisha kuwa kuna upungufu wa maji manispaa ya Tabora.

Sababu ya upungufu ni matengenezo ya bomba kubwa lililopasuka eneo la kanyenye barabara ya Jamhuri

Aidha maji ya KASHWASA hayajaanza kuingia kwenye tenki la Itumba.

Maeneo yote ya Manispaa ya Tabora yanaathirika isipokuwa baadhi ya mitaa katika kata ya Mpera yanayopata maji kutoka chanzo cha  Kazima.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya  Mkurugenzi Mtendaji-TUWASA

08/12/2023