UPUNGUFU WA HUDUMA Y...
UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI MAENEO YOTE YA MANISPAA NA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA UYUI (ISIKIZYA)
24 Oct, 2023

TANGAZO KWA UMMA

MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI TABORA (TUWASA) INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWEPO UPUNGUFU WA MAJI MAENEO YOTE YA MANISPAA NA MAKAO MAKUU YA WILAYA YA UYUI (ISIKIZYA)

HII NI KUTOKANA NA HITILAFU YA UMEME KWENYE MITAMBO YA UZALISHAJI MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA NA KUENDELEA KUPATA MGAO WA UMEME KWENYE MITAMBO YA UZALISHAJI IGOMBE / KAZIMA.

TUWASA INAOMBA WATEJA NA WANANCHI KUWA WAVUMILIVU WAKATI IKIENDELEA KUFUATILIA MATENGENEZO YA MITAMBO YA UMEME KWENYE CHANZO CHA MAJI YA ZIWA VICTORIA PAMOJA NA KUFUATILIA UNAFUU WA MGAO WA UMEME KWENYE VYANZO VYA IGOMBE NA KAZIMA.

TUWASA INASISITIZA WATEJA KUTUMIA MAJI KWA UANGALIFU KIPINDI HIKI CHA CHANGAMOTO.

IMETOLEWA NA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI

TUWASA.

24/10/2023