TANGAZO LA KUREJESHA HUDUMA YA MAJI BILA FAINI KWA WATEJA WALIOSITISHIWA HUDUMA YA MAJI
24 Jan, 2023
TUWASA inawatangazia wateja wake wote kwamba, kuna nafuu ya kurejesha huduma ya maji kwa wateja waliositishiwa huduma kuanzia mwezi Desemba 2022 hadi Julai 2022 .
Wateja wote waliopo katika kundi tajwa watarejeshewa huduma ya maji kwa kulipa madeni wanayodaiwa pekee bila kulipa 15,000 ya faini.
Tangazo hili litafikia ukomo tarehe 28.01.2023
Vigezo na Masharti vitazingatiwa
Karibuni sana.